Lowasa amtembelea Lissu kumjulia hali - KULUNZI FIKRA

Monday, 11 September 2017

Lowasa amtembelea Lissu kumjulia hali

Waziri mkuu wa zamani ,Edward Lowasa yupo Nairobi nchini Kenya kumjulia hali mbunge wa Singida mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika hospitali ya Aga khan, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Lissu ambaye ni mwanasheria wa chadema alijeruhiwa kwa risasi tano Alhamisi septemba 7 akiwa ndani ya gari, nyumbani kwake Area D mjini Dodoma akitokea Bungeni.

Katika akaunti yake ya Twitter, Lowasa ame- tweet  alisema " Earlier today I paid a visit at Nairobi hospital to see our MP, president of TLS and dear Friend @ Tundulissutz.He is recovering well. It is sad time for Tanzania. Let us all keep praying "

Kwa tafsiri isiyo rasmi amesema " Mapema leo nilitembelea hospitali ya Nairobi kumwona Mbunge, Rais wa (TLS) na Rafiki yangu kipenzi Tundu Lissu.Anaendelea vizuri. Ni kipindi cha masikitiko kwa Tanzania, kwa pamoja tuendelee kumuombea "

Katika twett hiyo, Lowasa ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, ameweka picha akiwa pamoja na Alice ambaye ni mke wa Lissu , mwenyekiti wa chadema, Freeman Mbowe na Dereva wa Lissu Simon Mohamed Bakari.

No comments:

Post a Comment

Popular