Jukwaa la Katiba Nchini (Jukata) limeandaa maandamano ya amani ya kutaka kurejeshwa kwa mchakato wa Katiba Mpya.
Akizungumza Jana Jumanne mara baada ya mkutano mkuu wa jukwaa hilo wa siku mbili ambao umeshirikisha mashirika yasaiyo ya kiserikali 184 nchini.
Meneja Programu wa Jukata, Machereli Machumbana amesema maandamano hayo katika ngazi ya kitaifa yanatarajiwa kupokelewa na Rais John Magufuli.
Amesema wamekubalina kufanya maandamano nchi nzima kuunga jitihada za Rais Magufuli katika harakati za kurejesha ari na heshima ya utumishi wa umma nchini ikiwa ni pamoja na jitihada zake za kupamba na rushwa, nidhamu na kulinda raslimali za Taifa ikiwemo madini.
“Katika pendekezo hili kutakuwa na ujumbe kuhusu Katiba Mpya na kwenye maandamano haya tumepanga Rais Magufuli ndiye awe anayapokea maandamano ya kitaifa kuhusu kumpongeza yeye na kumuomba akamilishe
mchakato wa Katiba ili jitihada zake ziwe na msingi, nguvu za kisheria kwa yote anayafanya,” amesema.
Amesema bila msingi wa kisheria jitihada zake hazitakuwa za kudumu na wao wanataka waweke misingi imara hata akitoka yeye akaja mwingine atabaki katika historia alinyoosha nchi na kuleta Katiba Mpya.
Pia amesema jukwaa hilo limekuwa na kawaida ya kuandika barua kukutana na viongozi wa kitaifa na kwamba wameandika barua kadhaa kwenda Rais Magufuli kujadiliana na kupata ushauri kutoka kwake kuhusu mchakato huo.
Tuesday, 26 September 2017
Home
Unlabelled
Jukwaa la katiba (JUKATA) kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza kurejeshwa kwa mchakato wa katiba mpya
Jukwaa la katiba (JUKATA) kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza kurejeshwa kwa mchakato wa katiba mpya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...

No comments:
Post a Comment