Watu sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia msikiti mkuu wa Igunga mjini, Mkoa wa Tabora na kumjeruhi mlinzi kisha kupora baadhi ya vitu vikiwemo vitabu vya dini ya kiislaam.
Mlinzi aliyejeruhiwa ni Juma Mussa (55),mkazi wa Mtaa wa Nkokoto ambaye amelazwa wodi namba nane katika Hospitali ya wilaya ya Igunga.
Akizungumza kwa shida akiwa wodini hapo mlinzi huyo alisema tukio hilo limetokea juzi saa 8.00 usiku ambapo watu hao walifika msikitini hapo kisha kurusha jiwe kwenye eneo alilokuwa amekaa.
Alisema baada ya kuona jiwe hilo aliamua kusimama ambapo jambazi mmoja aliruka uzio wa msikiti kisha kuingia na kuanza kumshambulia kwa mapanga kichwani.
Mussa alisema kwamba wakati akishambuliwa aliona watu wengine wakifungua milango ya msikiti huo huku mmoja wao akimwambia mwenzake kuwa "wewe maliza kabisa huyo mlinzi".
Hata hivyo mlinzi alisema kwamba aliendelea kuomba msaada wa kupiga kelele ili aweze kusaidiwa hali iliyosababisha majambazi hao kukimbia kusikojulikana.
Mhasibu wa msikiti mkuu wa Ijumaa wilaya ya Igunga, Issa Feruzi, alitaja vitu vilivyoibiwa ni Misahafu minne, feni moja, saa kubwa, vitabu vya hitma juzuu 30, kitabu cha mapato cha mapato na matumizi, Daftari za Tabligh nne, vipaza sauti, miswala miwili, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 374,000.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Igunga, Melchades Magongo, alikiri kumpokea Juma Mussa.
Tuesday, 26 September 2017
Home
Unlabelled
Igunga Tabora: Majambazi 6 wavamia msikiti na kumjeruhi mlinzi kisha kupora baadhi ya vitu vikiwemo vitabu
Igunga Tabora: Majambazi 6 wavamia msikiti na kumjeruhi mlinzi kisha kupora baadhi ya vitu vikiwemo vitabu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...

No comments:
Post a Comment