Jaji mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma aapishwa - KULUNZI FIKRA

Monday, 11 September 2017

Jaji mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma aapishwa

Leo Rais Magufuli amemuapisha jaji mkuu wa Tanzania, Profesa
Ibrahim Hamis Juma na ameongelea mpango mkakati wa kuboresha mahakama ikiwemo kuwafikia zaidi watanzania ikiwemo ujenzi wa gharama nafuu wa mahakama, anasema Tanzania inasifika kwa ujenzi wa mahakama nyingi kwa wakati mmoja duniani.

Amesema wanajenga mahakama zinazoendana na teknolojia ikiwemo tehama na anasema bahati nzuri amekuta watu wameshapanga mipango, yeye anatekeleza.

Jaji mkuu: Kuhusu mihimili mitatu, watu wanasema inaingiliana, hamna nafasi ya mgongano. Bila kushirikia hatutaweza kusaidia wananchi, kila mhimili una eneo lake. Ukielewa dhana kila mtu ana eneo lake, mihimili hii haigongani.

Serikali ni mdau mkubwa mahakamani, mwanasheria mkuu ana kesi nyingi mahakamani. Sisi tunajaribu kupunguza hiyo migongani. Huwa tunajaribu kuangalia majaji tukikutana serikali ya tano ilivyoingia, tumewekana mikakati kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji, madawa ya kulevya etc.

Tunajaribu kwenda ili tusicheleweshe juhudi za mhimili mwingine.

Palamagamba Kabuni: Awali ya yote nimshukuru mwenyezi mungu Rahim kwa ruzuku ya uhai na uhai, nikushuru Rais kwa kuiheshimu kata. Rais wa Nijeria alimteua jaji mkuu pia Rais wa Zambia alimteua jaji mkuu.

Bila ya shinikizo la mtu yeyote, mheshimiwa Rais imempendeza na kuona inafaa kumteua jaji mkuu wa nane wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ibrahim Juma nimemfundisha mwaka wa kwanza na kupata bahati ya kuwa semina leader wao. Ibrahim ni mtu wa Musoma, ukimtazama unaweza kudhani ni mtu dhaifu lakini ni very firm. Ulikuwa huwezi kwenda kufundisha darasa lao huku hujajiandaa, Prof. Ibrahim alikuwa anasoma.

Alipoajiriwa baada ya kumaliza ilikuwa afanye Land Law, tulipata fursa ya masomo ya islamic Law uingireza, tukaamua kumpeleka. Tulipeleka muislam mmoja na mkatoliki ataeenda kusoma Islamic law.

Rais Magufuli: Leo mimi ni furaha na nafikiri sina maneno zaidi. Nikupongeze sana kwa niaba ya serikali kukupongeza.

Ninafahamu kazi ya kuteua jaji mkuu ni kazi ngumu, kama kazi ya kumuhukumu mtu ilivyo ngumu. Ni hivyo hivyo nami nimeu-test ujaji kidogo kwa kumteua jaji mkuu.

Ilibidi nichukue muda wa kujiridhisha na ilibidi nitumie kipengele cha kumteua kaimu jaji mkuu, nilifanya hivyo si kwa sababu majaji walikuwa hawafai, sikutaka kumteua jaji na baada ya mwaka mmoja nimteue mwingine, au mwingine anastaafu.

Nilizingatia hayo, nilizingatia suala la rushwa wakati namteua jaji mkuu. Makamani, serikali kuna rushwa, kila mahali. Nilikaa na kumuomba Mungu nipate kiongozi anaweza kulisimamia hili kwa muda mrefu. Wapo majaji wengi wazuri lakini wapo waliokuwa wamebakiza muda mdogo, wanisamehe kama nimekosea.

Lengo lilikuwa kupata jaji mkuu atakaekaa muda mrefu hata miaka saba au nane. Prof Mungu ndie amekuchagua hivyo ukawatumikie watanzania. Nafahamu kuna changamoto nyingi kwenye makama ikiwemo bajeti finyu.

Changamoto ni nyingi, mimi na serikali ninayoiongoza tunazifahamu kama ilivyo kila sehemu. Ukishakuwa kiongozi katika nchi masikini kamaTanzania, laima uzikubali changamoto, maisha ni changamoto, lazima tuzikabilli katika kuzitatua.

Kazi nzuri yeyote lazima wapatikane watu wa kuponde, hata nilivyokuteua kaimu jaji waliponda sana. Tena inawezekana hata wengine walikuwa wanafunzi wao, wengine labda waikuwa vilaza. Walisahau ibara hio na watambue katika kuteua jaji mkuu sikuwa na shinikizo.

Naomba orodha ya watu waliohukumiwa kunyongwa msiniletee kwa sababu najua ugumu wake. Ikiwezekana siku moja ama mbili mkae hivi vyombo vyote vya kutoa haki mjadili changamoto. Kwa mfano unakuta mtu anakutwa na ushahidi wote lakini inashindikana kuhukumiwa kesi, labda kuna mmoja amechelewesha ushahidi etc.

Serikali itaendelea kutatua changamoto. Hapa sikuja kutoa hotuba, leo ni zamu yangu ya kukuapisha. Nitoe shukrani kwa jaji Chande na wengine kwa kazi kubwa walizozifanya katika kujenga misingi, jaji natumaini utaendelea kutumia busara zao.

Hawa majaji ni waadilifu sana. Huwezi kumsikia jaji Chande anazungumza chochote au majaji wengine. Tofauti na wastaafu wa sehemu nyingine, wanawashwa washwa sana. Nawapongeza sana waheshimiwa majaji.

Utusaidie jaji mkuu wanaoletwa huko kwako kwa rushwa wakiletwa huko kwako, hela nyingi zinapotea kwa sababu ya rushwa.

No comments:

Post a Comment

Popular