Chadema: Tunavitaka vyombo vya usalama vyote vitekeleze kazi zake kwa weledi kama vinavyofanya kwenye matukio mengine - KULUNZI FIKRA

Friday, 8 September 2017

Chadema: Tunavitaka vyombo vya usalama vyote vitekeleze kazi zake kwa weledi kama vinavyofanya kwenye matukio mengine

 Katibu mkuu wa chadema, Dkt Vincent Mashinji  amesema kabla yatukio hili lililotokea, Lissu alishawahi kusema kuwa anafatwa na ana hofu na maisha yake na alifatwa na gari Nissan Premio na akawa na wasiwasi kuwa maisha yake yako hatarini.

Safari: Chama chetu kilishapata misukosuko mingine kabla ya suala hili la Lissu ikiwemo kupotea kwa Ben Saanane zaidi ya miaka miwili imepita na hakuna kitu chochote positive kimefanywa na vyombo vya usalama.

Lingine ni kuuawa kwa Alphonce Mawazo, mwenyekiti wa CHADEMA Geita. Aliuawa vibaya sana na hata kuzikwa kwake ilikuwa fujo, makamanda wa polisi wakakataa hata kuagwa.

Sisi wanasheria kuna kipengele namba 122 kinaruhusu watu kufanya inferences kwamba dhana ni nini katika kadhia kama hii, dhana sio nzuri kwa hio tunaiomba polisi, jana Lissu gari yake imepigwa risasi 28-32 kulingana na makamanda. Sisi wanasheria unapotaka kuthibitisha, mauaji ya kukusudia ama ya kujaribu kuu kwa kukusudia unajiuliza vitu viwili vikubwa, silaha gani imetumika na imepiga mahala gani kwenye mwili.

Ukiangalia matukio ya ile gari, mpigaji alidhamiria kupiga kichwa na kifua cha Lissu. Kwa hio nia ya kutaka kuua ipo na silaha iliyotumika sio chini ya SMG. Kwa hio hali hii inatia simanzi.

Tunavitaka vyombo vya usalama vyote vitekeleze kazi zake kwa weledi kama ambavyo wanaweza kufanya katika matukio mengine.

Katibu mkuu(Mashinji): Nimesimama nikiwa na majonzi kwa sababu ni kama siku tatu tumekutana hapa na tuliongelea umuhimu wa kuwa na jamii inayoheshime sheria na katiba na nilionyesha wasiwasi wangu kuwa wale wanaojiona wana nguvu wanaweza kujiona wako juu ya sheria.

Mheshimiwa Lissu ni rais wa watetezi wa haki na wote wanaopenda haki itendeke, jana akiwa anatoka bungeni kuna gari ilimfata, alipofika nyumbani kwake walimshambulia risasi kama mnyama, tukio hili lilikuwa la kusikitisha na kufedhehesha na tunawashukuru waliokuwepo kwenye tukio kwa kuokoa maisha yake kwa kumpeleka hospitali ya Dodoma.

Tunawashukuru sana madaktari kwa jitihada zao zote walizozifanya za kuokoa maisha yake na mpaka asubuhi ya leo bado tuko nae hai, najisikia kidogo niko protected kwa sababu nami ni daktari pia na nilisoma emergency medicine waendelee na moyo huyo huyo.

Damu ya Lissu imemwagika nyingi sana na baada ya kupewa taarifa ya shambulio lake nilikosa cha kusoma baada ya kuambiwa idadi ya risasi zilizopenya kwenye mwili wake, kama mtaalam nilijua kinachoendelea kwenye mwili wake, nilikaa ofisini kwa masaa kadhaa nikitafakiri nini kitatokea. Hawajatutisha bali wametuimarisha zaidi. Na hawajatutisha wametuimarisha zaidi.

Tundu Lissu baada ya matibabu katika hospitali ya Dodoma iliamriwa aletwe Dodoma. Kutoka na hali ya kiusalama na tulichelewa kumleta muhimbili

Tulifanikiwa kumpandisha ndege na ndege hiyo ilimchukua saa 8 usiku na mpaka asubuhi hii, mwenyekiti ameachana naye akiwa anajitambua.

Kwasasahivi kikubwa ni kupigania uhai wake na yeye mwenyewe amepigania pumzi yake na amewashinda wale wote waliotaka kumuangamiza.

Kwakuwa damu ya Lissu imekanyaga ardhi kabla ya muda wake. Nawaomba makamanda wote tuende kwenye hospitali zetu tukachangie damu na hiyo damu yetu ikawe ishara ya kulikomboa taifa hili.

Niwaombe makamanda wetu wote nchi nzima muweze kukutana na kujadili hali ya usalama katika maeneo yetu.

Ili kuhakikisha mh Lissu anapata huduma bora za matibabu. Kwa wale wote watakaopenda kuchangia watumie akaunti yetu ya CRDB inaitwa kwa la msingi yaani CHADEMA M4C 01J1080100600.

Unaweza kuhamisha kwa njia ya simu.

Nawashukuru sana wabunge kwa ushirikiano wao walioonesha jana kwa kuhakikisha mwenzao anapata matibabu.

Mwisho, nipende kuwakumbusha, kuna watu maarufu sana kwenye hii nchi wanaitwa watu wasiojulikana. Waliwahi kumtokea mwandishi wa habari Absalim Kibanda wakammwagia tindikali, walimmwagia tindikali Saed Kubenea, walimteka Ney wa mitego, wamemteka Ben Saa Nane, walimteka Roma mkatoliki, wamempiga Lissu risasi, walimnyooshea Nape bastola. Sisi kama jamii tunatakiwa tuseme sasa hawa watu wanajulikana. Lazima tukutane tuanze kuwatambua.

Awamu iliyopita ilikuwa na kitu kinaitwa Polisi jamii. Lazima turudi kwenye asili yetu.
Tusiendelee kuaminishana kwamba hawa watu hawajulikani.

No comments:

Post a Comment

Popular