Yono wapiga marufuku kutembelea nyumba za Lugumi - KULUNZI FIKRA

Monday 21 August 2017

Yono wapiga marufuku kutembelea nyumba za Lugumi


 
 Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, kwa niaba ya TRA Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam ambayo imepewa dhamana ya kukusanya madeni ya wadaiwa sugu wa kodi imepiga marufuku yeyote kuingia katika nyumba za Kampuni ya Lugumi Enterprises zilizotangazwa kupigwa mnada Septemba tisa mwaka huu hadi hapo itakapotangazwa tarehe ya kuanza kukaguliwa, siku Kumi kabla ya mnada.

Nyumba hizo za kifahari ambzo ni maghorofa ziko katika maeneo tofauti ya jijini Dar es Salaam, moja Mtaa wa Mazengo, Upanga na mbili ziko Mbweni JKT katika wilaya ya Kinondoni na zinafaa kwa matumizi ya ofisi na makazi.

Mnada wa nyumba hizo unatokana na kampuni hiyo ya Lugumi kushindwa kulipa kodi ya serikali ya shilingi bilioni kumi na nne.

Mnada huo una masharti ambayo ni mnunuzi kulipa asilimia 25 ya thamani ya bei kwa atakayefanikiwa kununua nyumba hizo na kiasi kitakachobaki kulipwa ndani ya siku 14.

No comments:

Post a Comment

Popular