Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.
Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.
Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.
Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.
Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.
Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.
Monday, 21 August 2017
Home
Unlabelled
Sukuma: kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha presha Ndege kuzui
Sukuma: kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha presha Ndege kuzui
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
No comments:
Post a Comment