Mbunge wa Bunda mjini, Esther Bulaya apata dhamana na pia apewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa wa Mara,haki haijatengemaa - KULUNZI FIKRA

Monday, 21 August 2017

Mbunge wa Bunda mjini, Esther Bulaya apata dhamana na pia apewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa wa Mara,haki haijatengemaa

 
 Mbunge Bunda Mjini Ester Bulaya amepata dhamana kwa mashariti ya wadhamini watu na Tsh mil 20, amepewa rufaa ya kwenda Muhimbili kwa ajili matibabu zaidi.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara Joyce Sokombi (CHADEMA) amezungumzia hali ya Mbunge Mh. Ester Amos Bulaya, na kusema kwamba hali yake bado haijatengemaa kwani amepewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa, hivyo amewataka watanzania kumuombea.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Mh. Sokombi amesema presha ya Ester Bulaya ambaye ni Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini bado ipo chini, kiasi kwamba wameshindwa kumsafirisha kwenda hospitali kubwa, hivyo wanasubiri madaktari wamsaidie kurudisha hali ya presha yake, ndipo wamtoe hospitali.

 Pia Mh. Sokombi amesema kwa sasa Bulaya ameshapatiwa dhamana akiwa hapo hospitalini, lakini hawajajua hatma ya kesi kwani mpaka sasa hawajapewa maelezo ya sababu iliyofanywa ashikiliwe na polisi.


No comments:

Post a Comment

Popular