Watu 50 wazamishwa baharini - KULUNZI FIKRA

Thursday, 10 August 2017

Watu 50 wazamishwa baharini


Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, limesema mhalifu wa usafirishaji haramu wa binadamu aliwatupa zaidi ya wahamiaji 120 ndani ya bahari siku ya Jumatano wakati walipokaribia fukwe za Yemen.

Wahamiaji 50 kutoka Somalia na Ethiopia walizamishwa baharini kwa makusudi wakati msafirishaji haramu wa binadamu alipowatupa baharini karibu na fukwe za Yemen.
Hayo yamesemwa na shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa ni hali ya kushangaza na kinyume cha utu.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo wafanyakazi wake waligundua makaburi 29 ya wahamiaji katika ufukwe wa Shabwa. Maiti za wahamiaji hao zilizikwa na wenzao ambao walinusurika kufa.

No comments:

Post a Comment

Popular