Wanachama wa simba sc wapitisha mfumo wa - KULUNZI FIKRA

Sunday, 20 August 2017

Wanachama wa simba sc wapitisha mfumo wa

 
Wanachama 1,216 wa klabu ya Simba, leo Jumapili wamepitisha uamuzi wa klabu yao kuanza kuendeshwa kwa mfumo wa hisa.

Katika uamuzi huo ni mwanachama mmoja pekee ndiye alionyesha hisia zake kwa kupinga mfumo huo.

Wanachama bado wataendelea kubaki kuwa wamiliki wa klabu hiyo kwa asilimia 50 huku wawekezaji nao wakilimiliki kwa asilimia 50 pia.

Mabadiliko yaliyopitishwa na wanachama wa Simba yako hivi, wanachama watamiliki klabu yao kwa asilimia 50 huku 50 zikimilikiwa na wawekezaji.

Wawekezaji au mmoja, wawili au watatu watatakiwa kutoa Shilingi bilioni 20 katika uwekezaji huo, sawa na wanachama.

Kwa wanachama, kwa kuwa wanaonekana si wenye uwezo wa kutosha kifedha, wao watatakiwa kuchangia Shilingi bilioni nne tu ambazo ni asilimia 10 huku 40 ambayo ni bilioni 16 zitawekwa kando kwa kuangalia uwezo wao.

Suala la nani atakuwa mwekezaji itaundwa kamati baada ya watu kujitokeza, nayo itaandaa mkutano kuwaita wanachama kuwaeleza waliojitokeza katika uwekezaji huo ni kina nani.

Wawekezaji wanaweza kuwa wawili, watatu au vinginevyo na mgawanyo wa hisa kwa maana ya thamani na asilimia ndiyo utakaohusika.

No comments:

Post a Comment

Popular