Wabunge Tarime walaani kamatakamata ya wabun - KULUNZI FIKRA

Sunday, 20 August 2017

Wabunge Tarime walaani kamatakamata ya wabun

 
Wabunge katika majimbo ya Tarime Mjini na Tarime Vijijini mkoani Mara wamelilaumu jeshi
la polisi katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya kwa kumkamata mjumbe wa kamati kuu CHADEMA  na mbunge wa Jimbo la Bunda mjini, Esther Bulaya kwa kile kinachodaiwa kuhutubia katika jimbo lisilo lake na kusema kufanya hivyo ni kuzuia maendeleo kwa wananchi wa Tarime.

Agosti 18, mbunge  wa Tarime vijijini, John Heche alifanya mkutano wa hadhara katika mji wa Nyamongo mkutano ambao ulihudhuriwa na mbunge wa Jimbo la Bunda kwa nafasi yake kama mjumbe kamati kuu ya Chadema na kutoa mifuko 50 ya saruji katika kusaidia ujenzi wa bweni la wasichana.



Lakini mara baada ya mkutano huo kuisha hapo jana, polisi katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya walimkamata mbunge huyo na kulala rumande baada ya kukosekana kwa dhamana iliyotakiwa kutolewa baada ya kamanda wa Polisi katika mkoa huo wa kipolisi kutopokea simu ya kutoa amri ya kupewa dhamana.

Hatua hiyo ya kamatakamata inaonekana kuwachukiza wabunge wa majimbo haya ya Tarime na katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Esther Matiko, wabunge hao wamesema kuwa kufanya hivyo ni kuwanyima wana Tarime  Maendeleo.

Mpaka sasa mbunge huyo inaelezwa kuwa bado yuko rumande na keho atapandishwa mahakamani huku taarifa zaidi zikisema jeshi hilo linamtafuta mbunge wa Tarime vijijini ambaye alihutubia katika mkutano wa mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini ambalo si lake kiutawala.

                                                  

No comments:

Post a Comment

Popular