Serikali yampa siku 7 Tundu Lissu kukanusha habari ya kumhusisha Rais kwenye suala kukamatwa kwa ndege - KULUNZI FIKRA

Sunday, 20 August 2017

Serikali yampa siku 7 Tundu Lissu kukanusha habari ya kumhusisha Rais kwenye suala kukamatwa kwa ndege

Serikali, imesononeshwa na taarifa za upotoshaji zinazoendelea kutolewa na Mbunge wa Singida mashariki Mhe Tundu Antipas Lissu akielezea kwamba Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli alihusika kwenye kandarasi ya ujenzi wa barabara ya wazo-Hill Bagamoyo na kampuni ya striling Construction ya nchini Canada.
Serikali inapenda kuujulisha umma wa Tanzania kupuuza taarifa hiyo kwani ni ya uongo, na uzushi, yenye nia ya kuaribu amani na mshikamano wa Taifa ukweli ni kwamba mwaka 2009 Mhe Dkt John Pombe Magufuli hakuwa waziri wa ujenzi kama ambavyo Mhe Tundu Lissu ameeleza.Kipindi hicho Mhe Dkt John Magufuli alikuwa waziri wa maendeleo ya uvuvi na mifugo kwa hivyo akushiriki kwa namba yoyote katika kuvunja kandarasi hiyo kama inavyopotoshwa.
Waziri aliyevunja kandarasi hiyo ni Mhe Dkt Shukuru Kawambwa Aliyekuwa waziri wa miundombinu kwa wakati huo,wizara iliyokuwa na dhamana ya kushughulikia masuala yote yanayohusu kandarasi za ujenzi wa barabara, reli, na miundombinu mingine.Hata hivyo waziri Kawambwa alishauria na mamlaka yake ya uteuzi na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kabla ya kufikia maamuzi.
Hata hivyo basi serikali inatoa siku saba(07) kwa Mhe Tundu Lissu kuomba radhi na kufuta maneno yake ya uongo yanayomhusisha   Rais wa nchi katika sakata hilo.
Vile vile serikali inawataka wananchi waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho Serikali inafanya jitihada za kuwaletea maendeleo na kuhakikisha ndege hiyo inawasili nchi.
Tayari kiasi cha dola 12.5M kimelipwa kwa kampuni ya striling Construction kama malipo ya awali ili ndege hiyo iweze kuwasili nchini mapema wakati mazungumzo mengine yakiendelea.
Serikali inawataka wananchi kutokusikiliza kelele za wapinga maendeleo ambao furaha yao ni kuona serikali ikishindwa kila jambo na inaahidi kuendelea kusaidia watanzania wote hususani wananchi wanyonge katika kuwaletea maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Popular