Wabunge kusimamia mfumo wa kielektroniki - KULUNZI FIKRA

Monday, 28 August 2017

Wabunge kusimamia mfumo wa kielektroniki

 Kamati ya Bunge ya Bajeti imesema itaendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya kielektroniki kwa kuwa mfumo huo umeonyesha mafanikio.

Akizungumza leo Agosti 28 baada ya kamati kutembelea Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), mwenyekiti wake, Hawa Ghasia ameipongeza kampuni ya Maxcom kwa ubunifu.

Amesema kabla ya utaratibu wa malipo kwa njia ya kielektroniki fedha za Serikali zilikuwa zikipotea, hivyo kukwamisha maendeleo ya nchi.

“Napongeza kwa ubunifu huu, njia hii ya ukusanyaji mapato inatakiwa kuigwa na taasisi zote na wafanyabiashara,” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Maxcom Africa Plc,Jameson Kasati amesema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa kadi za malipo ya mabasi yaendayo haraka.

Amesema kwa sasa wananchi waendelee kutumia tiketi za kawaida na kadi zitakuwa tayari hivi karibuni.

“Kadi za mabasi yetu zitakuwa tayari hivi karibuni, endeleeni kutumia tiketi,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Popular