Kiongozi wa chadema aliyehukumiwa miaka mitano jela, aachiwa huru - KULUNZI FIKRA

Monday, 28 August 2017

Kiongozi wa chadema aliyehukumiwa miaka mitano jela, aachiwa huru

Diwani wa Kata ya Kiangasaga wilayani Tarime kwa tiketi ya CHADEMA mheshimiwa Kichinda almaarufu kama Mzee wa protocal amechiwa huru na mahakama baada ya mahakama kudai kuwa hana kosa lolote.

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amethibitisha kuachiwa kwa diwani huyo ambaye awali alikuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela katika mahakama ya wilaya ya Tarime kutokana na kesi ya kikatiba. Baada ya kukata rufaa mahakama ilibaini kuwa kiongozi huyo hakuwa na kosa lolote.

"Nikiwa na Mzee Kinchinda diwani wa CHADEMA kata ya Kiangasaga ambaye alihukumiwa na kufungwa miaka mitano jela, tukakata rufaa nashukuru mahakama kuu imemuachia huru na kusema hakuwa na kosa lolote na sasa ameruhusiwa kwenda kufanya kazi zake kuwakilisha wananchi waliomchagua. Hongera Mzee Kichinda" alisema John Heche

No comments:

Post a Comment

Popular