Uchaguzi mkuu wa 2020 wavuruga mchakato wa uchaguzi wa chadema - KULUNZI FIKRA

Thursday 31 August 2017

Uchaguzi mkuu wa 2020 wavuruga mchakato wa uchaguzi wa chadema

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amefuta mchakato wa kuwapata viongozi katika kanda za chama hicho, kutokana na zoezi hilo kuingiliwa na kambi zinazojiandaa kumweka mtu wao atakayegombea urais kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Taarifa hiyo imetolewa jana Alhamisi Agosti 31 na katibu wa CHADEMA, Dkt. Vicent Mashinji, ambapo pia inawataka wanachama wake kufuta maandalizi yote yaliyokwisha fanyika mpaka mwenyekiti Mbowe atakapoamua tena.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari kupitia mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene, Mbowe amefuta matokeo ya chaguzi zilizokwisha fanyika mwaka huu kutokana na uwepo wa misuguano ya vita ya urais wa mwaka 2020.

Katibu mkuu Dkt. Mashinji, ameutangazia umma wa CHADEMA, kuhusu uwepo wa mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho itakayokutana Septemba 2, mwaka huu, ili kupitisha jina la Onesmo Ole Nangole, kugombea tena ubunge Jimbo la Longido baada ya mahakama kuamuru uchaguzi urudiwe.

No comments:

Post a Comment

Popular