Tundu Lissu: wanaogopa kutumbuliwa - KULUNZI FIKRA

Saturday, 19 August 2017

Tundu Lissu: wanaogopa kutumbuliwa

 
 Rais wa (TLS), Tundu Lissu amefunguka na kusema wabobezi wa sheria nchini akiwepo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Waziri wa Katiba Na Sheria Prof Palamagamba Kabudi wanamsikitisha kwa kuwa wanashindwa kuishauri vizuri serikali

Tundu Lissu alisema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari na kudai kuwa wataalam na wabobezi wa sheria ndani ya serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao vizuri kuishauri serikali vizuri kuhusiana na masuala ya sheria jambo ambalo linaleta athari katika nchi, ikiwepo kuzuiwa kwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-Dash 8

"Bungeni kulijitokeza mjadala na nikazungumza lakini Dr Mwakyembe na Profesa Kabudi walinijibu kuwa sisi kama nchi huru hatuwezi kuogopa kushtakiwa katika mahakama ya Kimataifa kwa kuvunja mikatba na kuvunja wajibu wetu kwa Jumuiya ya Kimataifa kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa tulioisaini na ambayo sisi ni wanachama. Nisema hapa kwa masikitiko makubwa kabisaa wanasheria waliobobea ambao wanatakiwa kumuelekeza
Mhe. Rais sawa sawa wamekuwa hawatekelezi wajibu wao kwa sababu pengine ya kuogopa kutumbuliwa au kwa sababu zingine ambazo zipo kinyume na taaluma zao kabisa moja wapo wa ushauri wa namna hii ni hizi kauli kwamba hatutakiwi kuogopa kushtakiwa katika mahakama za kimataifa ni ushauri ambao ukitoka kwa mwanasheria unasikitika kabisaa" alisema Tundu Lissu

No comments:

Post a Comment

Popular