Mrithi wa Mpinga afuata nyayo za Magufuli - KULUNZI FIKRA

Saturday, 19 August 2017

Mrithi wa Mpinga afuata nyayo za Magufuli

 
Mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani Fortunatus Musilimu, amefanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo kikuu cha mabasi yanayofanya safari nje ya mkoa wa Mbeya na kufungia leseni za madereva saba kwa muda wa miezi sita.

Hatua ya kufungia leseni hizo imekuja baada ya kubainika kuwepo ukiukwaji wa sheria na taratibu za usalama barabarani, ikiwemo magari matano kubainika kuwa na mapungufu kwenye usukani pamoja na kufika kituo cha mwisho kabla ya muda halali uliopangwa.

Kamanda Musilimu alifika kituo hicho kilichopo jijini Mbeya mnamo saa 11, alfajiri na kisha kuanza ukaguzi.

Katika ukaguzi huo pia magari hayo matano yalibainika kuwa na uppungufu kwenye magurudumu, kitu ambacho kilimsukuma kamanda huyo  kuyazuia kuendelea na safari zake.

Utekelezaji wa zoezi hilo unatajwa kuwa na lengo la kupunguza ajali za barabarani zinazoonekana kukithiri nchini Tanzania.

Kitendo cha kufanya ziara hiyo ya kushtukiza, kinaweza kufananishwa na nyendo za rais John Magufuli, ambaye mara kadhaa ameshuhudiwa akifanya ziara katika ofisi mbalimbali za umma, pasi na kutoa taarifa.

No comments:

Post a Comment

Popular