Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Afisa habari wake, Haji Manara wamesema wamedhamiria kumpeleka Mahakamani Kiungo Pius Buswita ambaye alisaini mkataba wa kuichezea simba lakini akufanya hivyo na badala yake ameamua kutoa Lugha za uchochezi dhidi ya Klabu hiyo.
Manara amebainisha hayo baada ya kusikia maneno yasiyo ya kiungwana yakisemwa na mchezaji huyo kwa kuikashfu wekundu wa Msimbazi mara alipoadhibiwa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja kutojihuhusisha masuala ya mpira na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
"Niwataarifu kwamba sasa klabu imedhamiria kumpeleka Pius Mahakamani ikitaka kwanza irudishiwe fedha zake lakini vyombo vya sheria na vinavyohusika vichukue hatua stahiki kwa huyu mchezaji", alisema Manara.
Aidha Manara amesema hawakuwa na nia ya kumshtaki Buswita kwani waliridhika na kilichofanywa na TFF lakini kwa kutofahamu au kwa makusudi wapo watu wanaoendelea kuchochea jambo hili ili Simba ionekane na makosa huku akiwataka wana Yanga kuachana na lugha za kusema TFF inapendelea wekundu wa Msimbazi kwani suala linalofanyika ni haki.
Mchezaji Pius Buswita anayetarajiwa kufunguliwa mashtaka na Simba.
"Sasa niwaombe wenzetu wa Yanga wasipende kutumia Lugha TFF inapendelea, na najua inafanyika makusudi kuwatisha viongozi wa TFF, timu iliyozoea kubebwa au kupendelewa kwa hiyo inapata ugumu fulani kuona uongozi huu unatenda haki na wao hawataki haki, sisi tumesema uongozi wa TFF usitupendelee, hatutaki kupendelewa bali tunataka tutendewe haki, haki iliyofanyika kwa Buswita ifanyike kwa mchezaji mwingine yoyote iwe ya Simba au timu nyingine yoyote, " alisisitiza Manara.
Mchezaji Pius Buswita alifungiwa kifungo cha mwaka mmoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa kosa la kusaini mkataba kwa vilabu viwili kwa wakati mmoja jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kanuni za usajili.
Wednesday, 30 August 2017
Home
Unlabelled
Simba kumpandisha kizimbani mchezaji wake
Simba kumpandisha kizimbani mchezaji wake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment