Ridhiwani amkumbuka Ndesamburo - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 16 August 2017

Ridhiwani amkumbuka Ndesamburo

Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani,Ridhiwani Kikwete amekutana na familia ya marehemu Philemon Ndesamburo na kueleza namna mzee huyo alivyokuwa karibu naye.
Ridhiwani amesema kuwa aliwahi kuambiwa na mzee huyo kuwa anatamani kumuona anakuwa kijana mwenye mapenzi na vijana wenzake.
Ndesamburo aliwahi kuwa mbunge wa Moshi mjini kwa tiketi ya chadema na pia mwenyekiti wa chama hicho hadi alipofariki dunia miezi michache iliyopita.
Ridhiwani amesema hayo baada ya kwenda kuhani msiba nyumbani kwa marehemu  mkoani Moshi.
Akizungumza na baadhi ya ndugu na jamaa wa marehemu Ndesamburo,Ridhiwani amesema alikutana Mara ya kwanza ana kwa ana na kuzungumza na mzee huyo miaka kadhaa iliyopita, alipokwenda Moshi kumuona babu yake aitwaye mzee Semindu na pia alikutana naye tena kipindi cha bunge la katiba.
"Namkumbuka sana aliwapenda sana wabunge vijana hata akiwaona wamekuwa kimya sana aliwauliza kuwa vipi mbona uko mpole leo?" amesema.

No comments:

Post a Comment

Popular