Barabara ya Ngokolo Shinyanga imezibwa na wananchi wakidai kuchoka na vumbi kali linalosababishwa na cement iliyomwagwa kujenga lami
Mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga(Shinyanga Press Club) ambae pia mmiliki wa MALUNDE1 BLOG ,Kadama Malunde amekamatwa na jeshi la polisi alipokuwa akitekeleza majukumu yake kwenye tukio la Wananchi kufunga barabara mjini Shinyanga.
Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo katika mtaa wa Magadula Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ambapo wananchi waliamua kufunga barabara inayotoka hospitali ya rufaa mkoani Shinyanga kuelekea gereji ya Mohamed Trans, kutokana na kuchoshwa na vumbi kali linalotokea pindi magari yanapopita katika barabara hiyo.
Vumbi hilo kali linatokana na ujenzi wa muda mrefu wa barabara hiyo amabapo miezi sita iliyopita mkandarasi alichanganya mchanga na simenti na kumwaga katika barabara hiyo kasha kuitelekeza na hivyo kusababisha vumbi kali kupita linaloathiri shughuli na afya za wakazi wa eneo hilo


No comments:
Post a Comment