Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda Jumatano hii amekabidhiwa mradi wa maboresho ya mtaa Samora uliogharimu zaidi ya shilingi milion 840 zilizofadhidhiliwa na serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la maendeleo Japan (JICA) na Manispaa ya Ilaa uliokamilika kwa 100%.
Mradi huo umehusisha ujenzi wa sehemu za Maegesho, mapumziko ya watu,upandaji wa miti na Maua, maboresho ya mazingira, uwekaji wa alama za barabarani pamoja na maboresho ya mitaa kuanzia Makutano ya Barabara ya Samora na Morogoro ikienda sambamba na kupunguza msongamano.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Makonda amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuhakikisha majengo yote ya Gorofa eneo la Posta yanafungwa Taa na Runinga za Matangazo ili kupendezesha Mji na kuongeza mwanga nyakati za usiku.
Amesema katika nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani majengo marefu yamekuwa sehemu ya matangazo hususani nyakati za usiku na kufanya miji kupendeza hivyo hata Dar es salaam tunaweza kufanya hivyo ili kufikia azma ya Rais Magufuli kutaka Dar es salaam kuwa mji wa Biashara
Aidha amesema mradi huo utakuwa wa awamu ili kuhakikisha mitaa na maeneo ya wazi yanaboreshwa ilikuwafanya wananchi kuwa na maeneo mengi ya kupumzika na kubadilishana mawazo ikiwa ni maono yake ya Dar es salaam Mpya
Awali eneo hilo lililofahamika kama Kaburi Moja lilikuwa likitumika kama Choo, Maegesho holela na wakati mwingine likitumiwa kwa uhalifu na uchafu wa mazingira.
Amewataka wananchi kutunza vizuri eneo hilo ili liweze kuwanufaisha wengi huku akipiga marufuku wamachinga kutofanya biashara kwenye eneo hilo.
Aidha Makonda amesema anataka kuona vituo vyote vya daladala mkoa wa Dar es salaam vinaboreshwe kuwa vya kisasa na kuwa sehemu ya matangazo ili kupendezesha mji na kuchangia ongezeko la mapato
Wednesday, 16 August 2017
Home
Unlabelled
RC Dar azindua mradi wa maboresho ya mtaa wa samora
RC Dar azindua mradi wa maboresho ya mtaa wa samora
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...


No comments:
Post a Comment