Mapacha walioungana wafariki muhimbili - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 16 August 2017

Mapacha walioungana wafariki muhimbili

Watoto mapacha ambao walizaliwa mkoani Morogoro wakiwa wameungana maeneo ya tumboni wamefariki dunia ktk Hospitali ya Taifa Muhimbili walipokuwa wakisubiri matibabu na jaribio la kutenganishwa.

Habari za awali kuhusu watoto hao;

Watoto mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana mkoani Morogoro imegundulika kuna uwezekano wa kuwatenganisha

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa Upasuaji wa Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zaituni Bokhary alipokuwa akitoa majibu ya vipimo vilivyochukuliwa hospitalini hapo kwa takribani wiki nzima.

Daktari huyo amesema kuwa baada ya kufanya vipimo, imegundulika kuna uwezekano wa kuwatenganisha watoto hao mapacha.

Majibu hayo yamekuja siku chache baada ya pacha hao kupimwa vipimo vya radiolojia ikiwemo CT Scan, MRI, X Ray kipimo cha moyo (ECO) pamoja na vipimo vyote vya damu.

Watoto hao waliozaliwa katika hospitali ya Misheni ya Berega iliyopo Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, Julai 21 mwaka huu wamenaza kuchukuliwa vipimo mbalimbali vya awali kabla ya upasuaji huo.

No comments:

Post a Comment

Popular