Timu kabambe ya uchunguzi ikiongozwa na wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa itahakikisha kila senti iliyofichwa nje ya nchi inarejeshwa ili haki iweze kutendeka kwa wahusika.
Msako huo wa nchi za nje unatokana na kuwepo kwa taarifa za baadhi ya wanufaika wa mgawo wa mabilioni hayo kuwa walitoroshea fedha hizo barani ulaya na maeneo mengine mbalimbali duniani. Aidha, harakati hizo za uchunguzi zinalengo moja tu kwamba hakuna fedha inayohusishwa na tuhuma hiyo ambayo haitafikiwa ikiwa ni pamoja na zile zilizokuwa zikizungumziwa bungeni zilizochotwa kwenye benki kwa mifuko ya sandarusi na ile ya rambo.
Imeelezwa kuwa eneo kubwa ambalo limelengwa na uchunguzi huo ni bara la Ulaya ambako inasemekana ndio kuna kiasi kikubwa cha fedha kimehifadhiwa na wanufaika wa mgawo huo.
Mussa Misalaba Ofisa Mahusiano wa TAKUKURU amesema kuwa ni kweli tuna maofisa wetu wa TAKUKURU wamekwenda nje ya nchi kufuatilia fedha za Escrow, kwa sasa siwezi kutaja kuwa ni nchi gani hasa tunazozifuatilia maana huu ni uchunguzi. Hata hivyo, ameongeza kuwa taasisi hiyo ya TAKUKURU imeamua kushirikisha taasisi zingine za Kimataifa katika kuwachunguza zaidi baadhi ya watuhumiwa wa Escrow kama wamehifadhi fedha hizo nje ya nchi.
Wednesday, 16 August 2017
Home
Unlabelled
Mabilioni ya Escrow yaliyotoroshwa sasa kurejeshwa nchini
Mabilioni ya Escrow yaliyotoroshwa sasa kurejeshwa nchini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
No comments:
Post a Comment