Sumaye avuna wanachama wapya 50 ukonga - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 16 August 2017

Sumaye avuna wanachama wapya 50 ukonga


 Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani Kamanda Fredrick Tluway Sumaye leo amekabidhi kadi na kuwapokea wanachama wapya 51 katika Jimbo la Ukonga. Tukio hilo limefanyika leo Jumatano tarehe 16/08/2017 wakati wa Ziara ya Kamati Tendaji Kanda Jimboni hapo. ...
Akizungumza kwa niaba ya wenzake baada ya kurudisha kadi za CCM na kukabidhiwa za CHADEMA, aliyekuwa kada maarufu na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa kwa awamu tatu Bi. Joyce Temu amesema ameamua kujiunga na CHADEMA baada ya kukerwa na mwenendo wa Serikali ya awamu ya tano ambayo ni matokeo CCM kupoteza Dira.
Katika hatua nyingine kamanda Sumaye amemkabidhi kadi ya CHADEMA wakili Msomi Amani Taslima, Mtoto wa Mbunge Mstaafu wa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Popular