Mwanamke mmoja wameuawa na watu wasiyofahamika jijini Mwanza - KULUNZI FIKRA

Thursday, 17 August 2017

Mwanamke mmoja wameuawa na watu wasiyofahamika jijini Mwanza



 ILEMELA, MWANZA: Mwanamke mmoja amekutwa akiwa ameuawa na watu wasiyofahamika na mwili wake kutupwa kwenye nyumba ambayo haijamalizika kujengwa (Pagala) huku akiwa amefungwa kwenye mfuko wa sandarusi na kuzungushiwa nguo alizokuwa amevaa.

Mwili wa marehemu uliweza kuonekana mahali hapo baada ya watoto waliokuwa wakicheza eneo hilo kuona kifurushi kilichotupwa kwenye Pagala ndipo walipotoa taarifa kwa mama yao na baadaye kutoa taarifa kwa uongozi wa Mtaa pamoja na kituo cha Polisi.

Upelelezi unaendelea wa kuwatafuta watu waliohusika na mauaji ya mwanamke huyo kwa namna moja ama nyingine.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.

No comments:

Post a Comment

Popular