Mkurugenzi wa Yono Auction mart nataka Magufuli aongezewe miaka 20 baada ya muda wake kikatiba kumalizika - KULUNZI FIKRA

Friday, 18 August 2017

Mkurugenzi wa Yono Auction mart nataka Magufuli aongezewe miaka 20 baada ya muda wake kikatiba kumalizika

Mheshimiwa Yono Stanley Kevela ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Njombe CCM 2005- 2010 ameridhishwa na kasi ya Magufuli na anadai kuungana na mzee Mwinyi kutaka Magufuli walau atawale mihula minne.

Yono ndiye Mkurugenzi wa kampuni wa Yono Auction Mart iliyokabidhiwa jukumu la kudai kodi na kufanya Mufilisi kwa wadaiwa sugu wa serikali. Alitoa kauli hii asubuhi ya leo akihojiwa na TBC redio.

Ikumbukwe Dr Magufuli ameshakataa kuongeza mihula ya Urais. Yono pia amezungumzia mengi aliyoyakuta Italy ambapo alisema alipofika huko wazungu huwapokea watanzania kwa kuwaita Magufuli kutokana na Rais huyu kufahamika duniani kote kwa kasi yake.

Mheshimiwa Yono kwa sasa anafanya PhD UDSM licha ya kuendelea na biashara na kampuni yake.

No comments:

Post a Comment

Popular