Naibu waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Ilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kumtia nguvuni na kumfikisha mahakamani mkandarasi wa Kampuni ya Audancia na mshauri mtaalam wa kampuni ya O&A kwa kile kinachodaiwa kujenga mradi wa maji kwa kutumia vifaa visivyo na ubora .
Jafo ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa fundi sanifu wa wilaya hiyo Stephano Mzuli, katika ziara yake ya kukagua mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi million 300 huku ukishindwa kufanya kazi.
Katika hatua nyingine, Jafo amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kumpa orodha ya miradi inayosimamiwa na mkandarasi huyo, ili wafungiwe na wasipewe tena tenda za miradi ya serikali.
Jafo ametumia nafasi hiyo pia kutoa agizo kwa Halmashauri ya Chamwino kuhakikisha inafanya maboresho katika mradi huo ili uanze kutoa huduma ya maji kwa wananchi kabla ya Septemba 15 mwaka huu.
Ziara ya naibu waziri Jafo imeonekana pia kuwapa matumaini wakazi wa Kijiji cha Itiso ambapo mradi huo upo, kutokana na adha ya maji inayowakabili, ambao wamemshukuru kwa hatua aliyoichukua

No comments:
Post a Comment