Bombardiea iliyonunuliwa Canada kupigwa mnada baada ya serikali kushindwa kulipa deni - KULUNZI FIKRA

Friday, 18 August 2017

Bombardiea iliyonunuliwa Canada kupigwa mnada baada ya serikali kushindwa kulipa deni

NDEGE iliyonunuliwa na Rais John Magufuli, nchini Canada, aina ya Bombardier Q400, imekamatwa nchini humo na iko hatarini kuuzwa kwa mnada.

Taarifa kutoka Montreal, Canada na wizara ya mambo ya nje jijini Dar es Salaam zinasema, kukamatwa kwa ndege hiyo, kunatokana na kampuni moja ya ujenzi ya nchi hiyo, kuidai serikali ya Tanzania kiasi cha dola za Marekani 38 milioni (zaidi ya TSh.90 bilioni).

Gazeti hili (Mwanahalisi) limeona nyaraka kadhaa kutoka kampuni ambayo inaidai Serikali na ambayo imekamata Ndege hiyo ili kufidia fedha zake.

Chanzo: Mwanahalisi

No comments:

Post a Comment

Popular