Manusura wa ajali ya ya wanafunzi wa Lucky Vincent wawasili,walakiwa na RC wa Kilimanjaro - KULUNZI FIKRA

Friday, 18 August 2017

Manusura wa ajali ya ya wanafunzi wa Lucky Vincent wawasili,walakiwa na RC wa Kilimanjaro

 RC Anna Mghwira awaongoza wakazi wa Kilimanjaro kuwapokea wanafunzi watatu wa shule ya Lucky Vincent waliowasili asubuhi kutoka Marekani.

Wanafunzi watatu wa Shule ya Lucky Vincent waliokuwa wakipatiwa matibabu Marekani wamewasili nchini asubuhi hii katika Uwanja wa KIA.

Kwa mujibu wa mh. Lazaro Nyalandu ndege hii kubwa imekuja na vifaa tiba ambavyo vitasambazwa katika hospitali za serikali na binafsi.

Furaha imetawala ujio wa watoto watatu wa Shule ya Lucky Vicent waliowasili leo Ijumaa, Agosti 18 wakitokea nchini Marekani kwenye matibabu baada ya kupata ajali Mei mwaka huu.

Wazazi na ndugu waliruhusiwa kuingia ndani ya ndege hiyo kuwapokea watoto wao ambao wamepata nafuu kwa kiasi kikubwa.

Wilson Tarimo alikuwa wa kwanza kushuka katika ndege akiambatana na mdogo wake aliyeingia katika ndege kwa ajili ya kumpokea.

Baada ya hapo aliyefuatia ni Saidia Awadhi pili akifuatana na Doreen Mshana kushuka katika ndege hiyo iliyokuwa na wajumbe 16 ambao waliambatana na watoto hao.

Baada ya kushuka walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aliyeambata na viongozi wengine kutoka Mkoa wa Arusha.

Watoto hao wote wakati wanashuka walionekana wenye nyuso za furaha baada ya kukaa Marekani kwa miezi mitatu wakipata matibabu.

No comments:

Post a Comment

Popular