Mhe Agustino Mrema awafunda wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha NRA. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 30 August 2017

Mhe Agustino Mrema awafunda wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha NRA.

 
Chama cha NRA -National Reconstruction Alliance, kimefanya mkutano wake mkuu 27/8/2017 wa kuchagua viongozi wao wa kitaifa, kwa miaka mitano 2017/22.

Katika mkutano huo baadhi ya wageni waalikwa walikuwa ni Msajili msaidizi wa vyama vya siasa ndugu  Sisty Nyahoza, Mwenyekiti wa chama cha TLP na Mwenyekiti wa bodi ya Parole Mhe. Agustino Mrema, Katibu Mkuu wa TLP, Mhe Nancy Mrikaria, Katibu Mkuu wa chama cha AFP (mhe Rashidi Rai), Katibu Mkuu wa chama cha UMD (Mhe Moshi Kigundula), Mwenyekiti Taifa wa chama cha makini (Mhe. Mohamed Abdulla), Katibu Mkuu wa SAU (Mhe. Mwangosi).

Katika mkutano huo, NRA iliwachagua Mhe. Simai Abdullah kuwa Mwenyekiti Taifa na Mhe. Hassan K. Almas kuwa Katibu Mkuu. Katika kutoa salamu kwa wajumbe wa mkutano huo, Mhe. Agustino Mrema kwa niaba ya viongozi wengine aliwataka wanachama wa nra kuwa na uzelendo kwa nchi yao.

Alisema,"Lengo la kila chama ni kushika dola, laini hatiwezi kushika dola kwa pamoja, hivyo atakayeshika dola ni vyema sisi wengine kumpongeza na kumshauri vizuri ili awatimizie mahitaji watanzania", aliongeza kusema "Nchi imekuwa katika vita ya uchumi kwa sasa na juhudi mbalimbali zimefanywa tena zinaonekana wazi lakini kwa kuwa baadhi ya wanasiasa wamekosa uzalendo wamekuwa wakiwazodoa na kukejeli juhudi hizo"

Mhe. Mrema ambaye ni gwiji na mkongwe wa siasa hapa nchini alisema kuwa ,watanzania wamekuwa wakidanganywa kuwa yeye ni CCM, lakini aliwaeleza wananra kuwa yeye alitoka CCM tangu miaka 30 iliyopita lakini bado anazodolewa, lakini akawakumbusha kuwa Mhe. Edward Lowassa na Mhe. Frederick Sumaye wametoka CCM juzi (miaka 2) lakini hawaitwi CCM.

Hivyo alisema wanamwandama kwa kuwa ameonyesha uzalendo kwa nchi yake na hiyo ni character assassination, yeye yupo imara na ayaendelea kupigania Tanzania, lakini hakuishia hapo,alitoa mfano mwngine kwa kumtaja Mhe. James Mbatia ambaye aliteuliwa kuwa mbunge na Mwenyekiti wa CCM, lakini watu hawakumuita CCM.

Mhe. Mrema aliwakonga nyoyo wajumbe wa mkutamo wa NRA pale aliposema kuwa,"Yeye ni mwamba wa siasa za nchi hii hivyo hawezi kuwasikiliza wapiga kelele na kudai kuwa hao bado wanajifunza siasa"

Mhe. Mrema aliwataka wana NRA kutumia nafasi hii kuchagua viongozi shupavu na wazalendo. Mhe. Mrema alisema kuwa, NRA imeonyesha ukomavu kwa kufanikisha kufanya uchaguzi wao, pia aliwataka wajumbe kufanyia baadhi vifungu vya katiba marekebisho ili kupunguza idadi ya wajumbe wa mkutamo mkuu kwa kuwa imekuwa ngumu kwa vyama vingi kuingia katika hatihati ya kufutwa kwa tatizo la kuandaa mikutano mikuu.

Mhe. Mrema aliongeza kwa kuwaeleza wana NRA kuwa wamoja katika kipindi hiki cha kupata viongozi wao ili wasije kujutia ikiwa wataichechea fursa hii ya uchaguzi mkuu. Mhe Mrema, aliambatana na katibu wake Mkuu Mhe. Nancy Mrikaria na viongozi waandamizi wa chama chake.

No comments:

Post a Comment

Popular