Mahakama kuu imeiamuru tena serikali kumlipa mfanyabiashara wa Mwanza 14.7 bilioni - KULUNZI FIKRA

Wednesday 23 August 2017

Mahakama kuu imeiamuru tena serikali kumlipa mfanyabiashara wa Mwanza 14.7 bilioni

Mahakama kuu imeiamuru tena serikali kumlipa mfanyabiashara wa Mwanza 14.7billions.
MAHAKAMA kuu kanda ya Mwanza imeiamuru Serikali kuilipa kampuni ya Mansoor Oil Industries Ltd (MOIL) ya jijini Mwanza jumla ya 14.7billions kutokana na uamuzi uliotolewa na Waziri wa Ujenzi wa wakati huo John Pombe Magufuli kwa kutoa amri ya kuvunja kituo cha mafuta cha kampuni hiyo.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama kuu kanda ya Mwanza katika kesi ya madai namba 2 ya mwaka 2002 ambapo
kampuni hiyo ilikuwa ikiwashitaki Waziri Magufuli, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (wakati huo) Brigedia Hassani Ngwilizi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Katika kesi hiyo madai ya kampuni hiyo ya MOIL kwa serikali yalikuwa jumla ya 18bilions kutokana na kuvunjiwa kituo hicho cha mafuta kilichokuwa kimejengwa katika kiwanja namba 178 Kitalu eneo la Kirumba kando ya barabara ya Makongoro.

Katika madai hayo, kampuni hiyo iliomba kulipwa kiasi cha 593milions kama thamani ya jengo ambalo lilibomolewa kwa amri ya Waziri Magufuli, 13.4billions ikiwa ni kiasi cha faida ambacho ingekipata katika kipindi cha miaka 33 ambacho ilitarajiwa kufanya biashara na 4bilions kama hasara ya jumla ya mradi huo.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa July, 30 mwaka huu na Hakimu Mfawidhi H. Mushi kwa niaba ya Jaji Lawrence Mchome, mahakama ilisema baada ya kusikiliza pande zote ikiwa ni pamoja na kupitia vielelezo na ushahidi mbalimbali iliridhika na hivyo kutoa uamuzi kuwa mlalamikaji anapaswa kulipwa fidia katika madai yake.

Katika hukumu hiyo, Mahakama imesema kwamba mdai alikuwa na vibali halali vinavyoruhusu kuendesha shughuli zake katika eneo hilo, na kwa mujibu wa sheria, Rais ndiye alikuwa na uwezo wa kubatilisha vibali hivyo na si waziri.

Mahakama iliamuru Serikali Kuu kwa niaba ya washitakiwa watatu ambao ni Waziri Magufuli, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (wakati huo) Brigedia Hassani Ngwilizi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge kulipa fidia kama ifuatavyo.

Kuilipa kampuni hiyo kiasi cha fidia ya Sh 490 milioni badala ya Sh 593 milioni alizoomba, kumlipa Sh13.4 bilioni kama fidia ya faida ambayo angepata katika kipindi cha miaka 33 na kumlipa kiasi cha Sh 730 milioni ambacho ni sehemu ya Sh 4 bilioni aliyoomba kama hasara ya jumla katika mradi huo wa kituo cha mafuta.

Katika hukumu hiyo, mahakama imemwondoa mlalamikiwa mmoja ambaye ni Halmshauri ya Jiji la Mwanza kwa kuwa hakuhusika na uvunjaji wa kituo hicho. Pia mahakama imeamuru serikali kumlipa mdai huyo kiasi cha asiliamia 17% ya madai yake ya hasara ya jumla ya Sh730 milioni kwa mwaka tangu siku jengo hilo lilipobomolewa Juni 21, 2001 hadi siku ya hukumu ilipotolewa.

Makahama imeamuru kulipwa kwa mdai huyo tena kiasi cha asiliamia hizo 17% ya Sh13.4 bilioni kwa mwaka ambayo ni madai yake ya hasara kutoka siku jengo lilipobomolewa hadi siku ya hukumu.

Kituo hicho kilibomolewa wakati tayari kikiwa kimekaguliwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kutoa hati ya umiliki wa kiwanja hicho Na. 033005/167 ya muda wa miaka 33.

No comments:

Post a Comment

Popular