Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (Chadema) amesema kuwa baadhi ya madiwani waliojiuzulu na kukihama chama hicho hivi karibuni wamekiandikia chama hicho barua wakiomba kurejea.
Meya huyo wa Ubungo ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na kipindi cha Maisha Mseto cha 100.5 Times FM, ambapo ameeleza kuwa madiwani hao walirubuniwa kwa ahadi ya fedha ambayo hata hivyo haikutekelezwa kama walivyokubaliana baada ya kujiuzulu.
“Baadhi ya madiwani wametuandikia barua wanaomba kurudi, wanadhani labda wakirudi watarudi kwenye nafasi zao za udiwani kwa sababu ahadi walizokuwa wamepewa za fedha hazikutimizwa,” alisema Jacob.
Kiongozi huyo wa Chadema alidai kuwa kinachofanyika hivi sasa ni siasa za kununua wanachama kama ilivyo kwa vilabu vya soka kununua wachezaji kutoka katika vilabu pinzani.
Alipotakiwa kutoa ushahidi unaoonesha kuwa madiwani hao walipewa fedha na kiasi gani, alisema kuwa wakati wa kufanya mazungumzo walikuwa wanaitwa madiwani kadhaa na watu ambao alidai ni wa chama fulani, lakini baada ya mazungumzo wapo waliokataa mpango huo na kwamba ndiyo walitoa siri za majadiliano hayo.
“Sio kiasi kikubwa cha fedha, wengine waliahidiwa shilingi milioni 10 lakini baada ya kujiuzulu walipewa shilingi milioni tatu. Kuna mwingine aliadiwa shilingi milioni tatu na zikawekwa benki kabisa, lakini baada ya kujiuzulu fedha hizo ziliondolewa kwenye akaunti yake na benki ikamueleza kuwa aliyeweka ameieleza benki hiyo kuwa aliweka kimakosa hivyo alirejeshewa,” Jacob alidai.
Hata hivyo, alidai kuwa madiwani wa Dar es Salaam ‘hawajanunuliwa’ kwani wengi wanajitambua, wanamsimamo zaidi na wana uwezo wa kifedha angalau usiowafanya kurubuniwa kirahisi.
Jacob alisema kuwa kurejea uchaguzi kwenye kata ambazo madiwani hao wamejiuzulu kutaisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni kugharamia uchaguzi huku akitamba kuwa Chadema itarejesha nafasi hizo.
Zaidi ya madiwani kumi walijiuzulu nafasi zao miezi michache iliyopita na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wakieleza kuwa hawakushinikizwa na mtu yeyote bali wameridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli.
Friday 25 August 2017
Home
Unlabelled
Madiwani waliojiuzulu chadema waomba kurudi
Madiwani waliojiuzulu chadema waomba kurudi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya Mhe Freeman Mbowe na wenzake wanane ya kutaka kesi dhidi yao ipelekwe Mahakam...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment