Juvicuf yaunga mkono Baraza kuu Cuf, pia watoa maazimio yao - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 1 August 2017

Juvicuf yaunga mkono Baraza kuu Cuf, pia watoa maazimio yao





 KUH: KUUNGA MKONO MAAZIMIO YA BARAZA KUU.
JUVICUF Taifa inawapongeza kwa dhati kabisa Viongozi wake wote wa Chama cha Wananchi CUF kwa kuacha shughuli zao na kukutana kwa siku mbili katika Ofisi za Chama Vuga mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili muendelezo wa hujma zinazofanywa na dola dhidi ya CUF.

Nyote mutakumbuka kua Wajumbe wa Kamati ya Utendaji walikutana kwa ajili ya kikao cha Kamati ya Utendaji mnamo siku ya Alhamis tarehe 27/07/2017 na kukutana tena siku ya Ijumaa kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu ambapo baada ya kikao hicho Baraza Kuu lilitoa Maazimio kadhaa juu ya kile alichokiita Lipumba "Kuwafukuza Uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum wa Chama cha Wananchi CUF".

JUVICUF pamoja na kuwapongeza Viongozi weke pia inaunga mkono Maazimio yote yaliyotolewa na Baraza Kuu. JUVICUF inaamini kua Maazimio hayo yameleta matokeo Chanya kwa Wanachama, Wapenzi wa CUF na Watanzania kwa ujumla hasa baada ya wengi wao kufadhaishwa na kile alichokifanya Speaker wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Nd. Job Ndugai ambapo bila ya aibu aliamua kubariki uharamu wa Lipumba na genge lake.

JUVICUF umeutazamia uhuni huo uliofanywa na Lipumba na genge lake kwa msaada mkubwa wa dola kwa macho ya karibu sana na inapenda kuwajuilisha Viongozi wake wa Chama, Wanachama na Watanzania yafuatayo;

MAAZIMIO YA JUVICUF
JUVICUF  kwa sasa haitokubali tena kuona uhuni huu ukiendelea kufanyika na itachukua hatua madhubuti kwa wale wote wanaoshiriki kutekeleza hujma dhidi ya Chama chetu.

JUVICUF kabla haijachukua hatua ambazo inapanga kuzichukua kwa wale wote wanaosababisha hujma hizi inamtahadharisha Raisi Magufuli juu ya muendelezo wa mihimili yake katika kutekeleza hujma dhidi ya CUF. JUVICUF inafahamu fika kuwa yanayoendelea kutokea kuhusu CUF ni muendelezo wa ushahidi kuwa hujma dhidi ya Chama chetu ni mkakati mahususi wa kukipunguzia nguvu na kukifuta chama hiki ambacho kimekua mwiba mkubwa kwa upande wa Zanzibar na hatari zaidi umoja  wake na nguvu inayopatikana katika  UKAWA ,lakini pia ni chma chenye Wanachama /wafuasi  na mtandao wa kiuwakilishi ulioenea pembe zote za nchi nzima Bara na Zanzibar kwa kitaifa.

JUVICUF kwa sasa imeshachoshwa na upuuzi unaofanywa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi na maslahi ya wale wanaowatuma. JUVICUF inadhani pasi na shaka yoyote kua Raisi Magufuli na dunia haijawahi kushuhudia Tanzania ikichafuka ila hujma hizi zikiendelea kufanywa watashuhudia.

JUVICUF iko tayari kukilinda Chama na kulinda maslahi ya Wanachama wake na Watanzania kwa ujumla kwa gharama yoyote ile ikibidi hata kufa. Tukumbuke kua wenzetu wengi walishapoteza maisha kwa ajili ya kupigania maslahi ya Watanzania kupitia Chama cha Wananchi CUF, hivyo sisi hatutokua wa mwanzo na hatutokua tayari kuisaliti damu ya wale waliopigania maslahi hayo kama haki itazidi kuminywa.

JUVICUF inapenda kuwaarifu Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF na Watanzania kwa ujumla kua sasa inaandaa utaratibu wa kupambana na hujma za Lipumba kwa Vitendo. JUVICUF haiko tayari kuona kila siku Katibu Mkuu wetu na Viongozi wake wanasumbuliwa na kikundi cha watu 8 kinacholindwa na dola. "Enough is enough ".

Mwisho kabisa JUVICUF kwa mara nyengine tena inawapongeza Viongozi wote na inaunga mkono Maazimio yote ya Baraza Kuu na inawaomba Wanachama wasitetereke na waendelee kua wastahamilivu na kuwaskiliza Viongozi wao ila tunataka umakini na uadilifu kwa wale wenye majukumu yakiwemo ya kimkakati.

Abeid Kh. Bakar
N/M/Habari na Uenezi
JUVICUF Taifa
juvicufhabari@yahoo.com

No comments:

Post a Comment

Popular