Korea Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa mafupi , jeshi la Marekani limesema. Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo moja katika mkoa wa kaskazini wa Gangwon na kuruka kwa umbali wa kilomita 250 kulingana na maafisa wa Korea Kusini.
Tangu ifanyie majaribio kombora lake la masafa marefu mwezi uliopita, Pyongyang imetishia kurusha makombora yake katika kisiwa cha Marekani cha Guam. Lakini jaribio hili la hivi karibuni linajiri kufuatia zoezi la kijeshi la pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini.
Maelfu ya wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini wanaendelea kufanya zoezi la pamoja ambalo hufanywa kwa kutumia Komyupta.Marekani awali ilikuwa imeripoti kwamba makombora mawili yalikuwa yamefeli , lakini kulingana na tathmini yake mojawapo ya makombora hayo lililipuka wakati huohuo liliporushwa huku mengine mawili yakiruka kwa umbali wa kilomita 250 yakielekea maeneo ya kaskazini mashariki. Makombora hayo yalirushwa kwa tofauti ya dakika 30 , kulingana na afisa mmoja. Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini ilisema: Jeshi linaangalia kwa umakini hatua ya Korea Kaskazini ya uchokozi.
Saturday, 26 August 2017
Home
Unlabelled
Jeshi la Marekani limesema Korea kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa mafupi
Jeshi la Marekani limesema Korea kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa mafupi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
No comments:
Post a Comment