Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya juu kusini imepanga kuwafukuza madiwani wake 6 wa jimbo la Iringa mjini.
Hatua hiyo imefikiwa katika kikao kilichoisha hivi punde kilichokuwa kikijadili mwenendo wa madiwani hao ambao kwa muda mrefu wametuhumiwa kutokuwa kambi ya Msigwa ambae ni Mbunge na Mwenyekiti wa CHADEMA wa kanda hiyo.
Madiwani hao waliotuhumiwa pia kutumiwa na viongozi wa CCM kukwamisha shughuli za mbunge wa Iringa mjini Mhe Msigwa wanatarajia kuzungumza na waandishi wa habari leo

No comments:
Post a Comment