Fedha taslimu kiasi cha shilingi laki mbili zilizokua kielelezo katika kesi ya kuomba na kupokea rushwa inayomkabili afisa wa polisi mkoani Njombe zimeibiwa Mahakamani wakati kesi ikiendelea.
Afisa huyo ambaye aliomba rushwa mjini Moshi, alikamatwa na maafisa wa TAKUKURU na kesi yake kusikilizwa ktk mahakama ya Hakimu mkazi Moshi. Taarifa kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa fedha hizo ziliibiwa jumatano ya August 9 mwaka huu wakati kesi hiyo ikisikilizwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah amedhibitisha kupotea kwa fedha hizo na kueleza kuwa TAKUKURU inawahoji baadhi ya maofisa kadhaa wa jeshi la polisi juu ya suala hilo.

No comments:
Post a Comment