Tume ya IEBC imesema kuwa hakuna udukuzi wowote uliofanyiwa mfumo wake wa kutoa matokeo ya uchaguzi kielektroniki.
Afisa mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema kuwa mfumo huo uko salama.
Akivihutubia vyombo vya habari katika makao makuu ya IEBC katika eneo la Bomas jijini Nairobi, amesema kwamba mfumo huo haukuingiliwa kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi.
Amesema kuwa madai ya upinzani kwamba mfumo huo ulidukuliwa ili kumsaidia rais Uhuru Kenyatta kupata ushindi hayana msingi wowote.
Amesema kuwa maafisa wa tume hiyo waliufanyia uchunguzi mfumo huo hususan funguo zake na wakati kwamba hakuna tatizo lolote.
''Hakuna mtu aliyepewa funguo za kuingia katika mfumo huo hadi siku moja labla ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa kuna maadili',alisema Chiloba.
Hatahivyo amesema kuwa tume hiyo imeweka ulinzi mkali dhidi ya wadukuzi.
Tume ya uchaguzi Kenya yatoa fomu za matokeo
Upinzani kuhesabu kura katika uchaguzi Kenya
Mabalozi: Wanaowania Kenya wakubali uamuzi wa wananchi
Odinga: Mitambo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa
''Iwapo una ripoti zozote kuhusu vitisho vya mfumo wetu tushirikiane kwa sababu mfumo huu sio wetu bali ni wa raia wa Kenya'',aliongezea.
Bw Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC.
Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia, wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake.
Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia.
IGAD tayari imesema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa njia ilio huru na haki
Wednesday, 9 August 2017
Home
Unlabelled
IEBC yasema mfumo wake haukudukuliwa
IEBC yasema mfumo wake haukudukuliwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
No comments:
Post a Comment