Heche alia na Acacia kuhusu fidia za - KULUNZI FIKRA

Saturday, 19 August 2017

Heche alia na Acacia kuhusu fidia za

 
Mbunge wa Tarime vijijini John Heche, ameonesha kusikitishwa na kitendo cha mgodi wa North Mara, unaomilikiwa na kampuni ya madini ya Acacia, kushindwa kuwalipa fidia wananchi wa Nyamongo baada ya kuwahamisha kwenye maeneo yao.

Mbunge huyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameonesha masikitiko yake hayo jana jioni, wakati akihutubia umati wa wakazi wa Nyamongo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika maeneo mbalimbali ya jimbo lake.

Kwa mujibu wa taarifa wananchi walitakiwa kuhama maeneo yao kutokana na tathmini iliyofanywa na mgodi huo kwakuwa walikuwa karibu na eneo hilo la machimbo.

Mbali na hao waliokuwa karibu na mgodi, pia kulikuwa na maeneo ambayo North Mara iliyahitaji kwaajili ya shughuli za uchimbaji madini na kulazimika kuwazuia wananchi kutoendelea na shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo.

Inaarifiwa kuwa tathmini kadhaa zimeshafanyika kwaajili ya kujua thamani halisi ambayo mgodi huo wa North Mara unatakiwa kuwalipa wakazi hao, lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji wowote uliofanywa na wachimba madini hao.

No comments:

Post a Comment

Popular