Zitto kabwe: Serikali kubalini kuhojiwa na kutoa majibu, ni wajibu wetu kuhoji - KULUNZI FIKRA

Saturday, 19 August 2017

Zitto kabwe: Serikali kubalini kuhojiwa na kutoa majibu, ni wajibu wetu kuhoji

 
 Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuwa ni wajibu wao kuhoji na pia Serikali ni wajibu wao kutoa majibu huku akisema yeye binafsi hawezi kuhujumu nchi yake.

"Ni wajibu wetu kuhoji. Ni wajibu wa Serikali kutoa majibu. Mimi binafsi siwezi hujumu nchi yangu aslani. Kubalini KUHOJIWA",aliandika Zitto kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kauli hiyo ya Zitto Kabwe, inakuja baada ya Bi Zamaradi Kawawa kusema kuwa, Serikali imesikitishwa na ushiriki wa Wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Popular