Freeman Mbowe: Ni upumbavu kutumia zaidi ya milioni mia saba kufanya uchaguzi wa madiwani walionunuliwa na ccm. - KULUNZI FIKRA

Friday, 11 August 2017

Freeman Mbowe: Ni upumbavu kutumia zaidi ya milioni mia saba kufanya uchaguzi wa madiwani walionunuliwa na ccm.



Mwenyekiti wa (CHADEMA) na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe amefunguka na kusema ni upambavu mkubwa kutumia zaidi ya milioni mia saba kwa ajili ya kufanya marudio ya uchaguzi wa udiwani wa kata tatu baada ya madiwani wa CHADEMA kudaiwa kununuliwa na CCM. Mbowe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na wakazi wa Machame Uroki akiwa kwenye ziara yake jimboni Hai na kusema fedha ambazo zinakwenda kwa ajili ya uchaguzi wa marudio zingeweza kufanya mambo mengine ya msingi.


"Gharama ya kurudia uchaguzi wa diwani mmoja ni shilingi milioni mia mbili hamsini, madiwani watatu waliopewa fedha wakaikimbia CHADEMA wakawaacha wananchi huo ni usaliti gharama ya kurudia uchaguzi kwenye kata tatu ni milioni mia saba na hamsini. Hizi ni pesa zenu, hizi ni pesa za Watanzania pesa hizi zingetumia kujenga shule ya msingi kwa Kasagile, hizi ni pesa zingetumika kujenga barabara, tunaacha kujenga hospitali tunakwenda kuzitumia fedha hizi kwenye uchaguzi milioni mia saba na hamsini ni upumbavu mkubwa" alisema Mbowe

Hata hivyo Mbowe amesema kuwa licha ya madiwani hao kununuliwa hata uchaguzi ukifanyika kesho anaamini kuwa chama chake kitaibuka na ushindi kwa kata zote tatu
kaka mkuu.

No comments:

Post a Comment

Popular