Zitto awapiga dongo wapinga maendeleo - KULUNZI FIKRA

Saturday, 22 July 2017

Zitto awapiga dongo wapinga maendeleo




                                         
Mbunge wa Kigoma mjini ambaye pia ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, amewabeza baadhi ya watu wanaoitakia mabaya nchi hasa katika suala zima la maendeleo kutokana na utofauti wa itikadi za vyama.

Zitto amesema hayo leo Jumamosi Julai 22, mbele ya rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika uliopo mjini Kigoma.

Mbunge huyo pekee wa ACT,    amempongeza rais Dkt. Magufuli kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa raia wa Tanzania na kusema kuwa mtu yeyote anayejaribu kurudisha nyuma maendeleo kwa kigezo cha vyama, anastahili kupingwa vita kwa nguvu zote.

Siku za hivi karibuni Zitto amekuwa akitumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuwakosoa baadhi ya wanasiasa wanaojaribu kutoa matamshi yenye kuzitaka jumuia za kimataifa kutoipatia misaada ya kimaendeleo Tanzania.

Maneno aliyotamka leo yanaweza kutafsiriwa kama sehemu ya kuonesha msisitizo wa kile ambacho amekuwa akikiandika kwenye mitandao hiyo ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Popular