Kesho Jumanne kutakuwa na tukio la aina yake katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Pwani ambako Mlimbwende wa Tanzania 2006 Wema Sepetu anatarajiwa kufunguka aliyokuwa nayo Moyoni kwa muda mrefu mbele ya Vyombo vya Habari. Tukio hilo litashuhudiwa na Mwenyekiti wa Kanda kamanda Fredrick Sumaye pamoja na Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa kamanda Halima James Mdee (MB).
Pia, katika tukio hili adhimu Kamanda Wema Sepetu ataambatana na Mama Wema pamoja na Mashabiki wake.
Muda: Saa 5 kamili asubuhi.
No comments:
Post a Comment