Mbowe apinga wawekezaji kunyang'anywa viwanda - KULUNZI FIKRA

Monday, 31 July 2017

Mbowe apinga wawekezaji kunyang'anywa viwanda

Mwenyekiti wa chadema,Freeman Mbowe amesema serikali haiwezi kujenga viwanda peke yake bila kuihusisha sekta binafsi ambayo ndiyo mdau mkuu katika uwekezaji nchini.
Mbowe amepinga kusudio la Rais Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji viwanda walivyobinafsishiwa kwa madai kwamba serikali ilitakiwa kutafuta chanzo cha kufungwa kwa viwanda hivyo kabla ya kufikia uamuzi wake.
Mwenyekiti hiyo amebainisha sababu mbalimbali zilizofanya viwanda hivyo visifanye kazi kuwa ni pamoja na kutopatiwa ruzuku na serikali, teknolojia ya zamani ya viwanda hivyo na wakati viwanda hivyo vinajengwa kulikuwa na mfumo hodhi wa soko.
"Hakuna mfanyabiashara duniani ambaye atapewa kitega uchumi kinachozalisha halafu akakifunga .Hayupo!"
Amesema Rais Magufuli  hana mapenzi na sekta binafsi kwa kuwa anaamini kwamba kila mtu aliye kwenye sekta binafsi ni "mpiga dili"

No comments:

Post a Comment

Popular