Wakati mchakato wa uchaguzi ukiendelea ndani ya ccm kuwapata viongozi wapya wa ngazi zote,wajumbe wa kamati ya siasa ya kata ya kidatu mkoani Morogoro wamejiuzulu kwa madai ya kushindwa kutimiza wajibu wao wa uongozi.
Wajumbe hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kata hiyo,Magungu Alex waliachia ngazi muda wao wa uongozi wa miaka Kitano ukiwa tayari umemalizika.
Kwa mujibu wa katiba ya ccm,uchaguzi ndani ya chama hicho huwa unafanyika kila baada ya miaka mitano,waliojiuzulu waliingia madarakani mwaka 2012.
Katika taarifa ya katibu wa Itikadi na uenezi wa ccm,Humphrey Polepole aliye kwenye ziara ya kuimarisha chama hicho na kukagua maendeleo ya uchaguz,wajumbe hao waliachia ngazi baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wanachama kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao ikiwamo kutosimamia ipasavyo uchaguzi unaoendelea.
Polepole alisema sababu nyingine ya kujiuzulu kwao ni kushindwa kusimamia rasilimali za chama hicho,usaliti wakati na baada ya uchaguzi na tuhuma za kuisababishia kata hiyo ishindwe kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
"Haipaswi wakati wowote kugeuza chama hiki kuwa chama cha viongozi, yangu awali msingi wa kuanzishwa kwake kiwe chama cha wananchi kinachoshughulikia shida za watu," alisema.
Baadhi ya wanachama,walisema viongozi wamechelewa kufanya hivyo kwa sababu muda wa uongozi wao ulikuwa umeshamalizika.
Sunday, 30 July 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
-
Tanzania imechanua na kufanya vizuri katika viwango vilivyotolewa na mfuko wa Mo Ibrahim uliopima hali ya utawala bora na maendeleo na ku...
No comments:
Post a Comment