Mbunge wa Iringa mjini (chadema) Mchungaji Peter Msigwa amekosoa uendeshaji wa bunge,akisema sipika Job Ndugai ameshindwa kukisimamia chombo hicho,badala yake ananyanyasa wapinzani.
Hata hivyo,sipika Ndugai amemjibu Msigwa akisema hayo ni mawazo yake na kwamba mbunge huyo ni miongoni mwa viongozi wa bunge,hivyo kama kuna upungufu na yeye ni sehemu yake.
Mchungaji Peter Msigwa amedai kuwa Ndugai anaongozwa na serikali.
"Tunachomlaum Ndugai ni kwamba ametekwa na state(serikali) kiasi kwamba bunge la Tanzania limegeuka kuwa rubber stemp(mhuri)" amesema mchungaji Huyo wa kanisa la vineyard.
"Kwa hiyo,(Bunge) kuwapo pale ni kumaliza pesa za wananchi kwa sababu hakuna mahali ambako Bunge linaikosoa serikali.
Meno pekee ya Bunge linayo ni kuwatoa wapinzani ndani ya Bunge.
Pamoja na kusema hayo ,Mchungaji Msigwa si mmoja kati ya wabunge wa upinzani ambao wamekumbana na adhabu Kali za Bunge ambazo zimekuwa zikitolewa na kamati ya haki,maadili na madaraka ya Bunge inayoongozwa na mbunge wa Newala (ccm) George Mkuchika.
No comments:
Post a Comment