Maalim Seif amjia juu Ndugai - KULUNZI FIKRA

Thursday, 27 July 2017

Maalim Seif amjia juu Ndugai

Karibu mkuu wa chama cha Cuf maalim Seif Sheriff Hamad amesema kwamba hatua ya spika kuwavua ubunge udiwani na kuteua wengine wapya inalenga kudhoofisha mambo ya wabunge wa cuf na ukawa.
Amesema watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hicho kinachoitwa 'kuwafukuza uanachama'hatua kama hiyo haikufuata taratibu zote za kisheria na kanuni za Bunge kujiridhisha kwanza
"Spika Job Ndugai anadhani watanzania ni vichaa wamuamini kuwa alishachukua hatua za kujiridhisha kuwa wabunge wanane wa chama cha wananchi(cuf) wamefukuzwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo amekosa sifa za kuendelea na ubunge ndani ya Sikh moja?" Amehoji Maalim Seif
Amesema spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hawakuwasiliana na katibu mkuu wa chama ambaye kwa mujibu wa katiba ya cuf ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye katibu wa vikao vya mkutano mkuu wa taifa na baraza kuu la uongozi la taifa la chama?
Amesema yeye kama katibu,alimwamuandikia spika Ndugai barua,jumanne julai 25 akimweleza kwamba hilo lililoitwa baraza kuu la uongozi la cuf halikuundwa na wajumbe halali wa baraza kuu.
"Angekuwa na nia ya kweli ya kutaka kujiridhisha si hapo ndipo pangekuwa pa kuanzia kwa kuwepo kile kinachotiliwa shaka"amehoji.
Amesema spika Ndugai aliyapunguza hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa wa Dola wa kuhujum cuf na kuua demokrasia Tanzania.Hapo ndipo spika Job Ndugai alipolifikisha bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Popular