Mwenyekiti wa CCM afunguka kuhusu kifo cha Mdogo wake Heche. - KULUNZI FIKRA

Thursday 3 May 2018

Mwenyekiti wa CCM afunguka kuhusu kifo cha Mdogo wake Heche.

 
Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara kimelaani madai ya askari polisi kumuua kwa kumchoma kisu Suguta Chacha ambaye ni mdogo wake  na Mbunge wa Tarime vijijini (Chadema), Mhe John Heche.

Akizungumza Leo Alhamisi Mei 3, 2018, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye amesema haiwezekani raia anayekamatwa kwa tuhuma yoyote kufariki kwa kipigo au sababu yoyote siyohusika na ugonjwa wa kawaida akiwa mikononi mwa polisi.

"Nikiwa kiongozi na rafiki wa familia nalaani kitendo kilichofanywa na askari aliyefanya tukio hilia," amesema Kiboye alipotoa salaamu wakati wa ibada ya mazishi ya kijana huyo inayoendelea muda huu.

Kiboye amesema kwa nafasi yake ya uenyekiti wa mkoa, ataendelea kuwahimiza watendaji wa Serikali, vyombo na taasisi zake  kutekeleza wajibu na majukumu yao kwa weledi wakizingatia sheria, kanuni na taratibu.

No comments:

Post a Comment

Popular