Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa wa Dodoma imesema mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) Taifa ndugu Sadifa Juma Khamisi atafikishwa mahakamani kesho.
Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma Emma Kuhanga amesema Ndugu Sadifa atafikishwa mahakamani kesho Jumatatu Desemba 11, 2017.
Amesema mwenyekiti huyo wa UVCCM Taifa alikamatwa nyumbani kwake akiwapa soda wajumbe wa UVCCM kutoka mkoa wa Kagera kitendo ambacho ni kinyume na maadili.
UVCCM Taifa leo jumapili Desemba 10, 2017 inachagua viongozi wapya wa ngazi ya Taifa watakaongoza jumuiya hiyo ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano.
Ndugu Sadifa ambaye pia ni Mbunge wa Donge Zanzibar amekamatwa nyumbani kwake mailimbili mjini Dodoma
Aidha Kuhanga akithibitisha kukamatwa kwa mwenyekiti huyo wa UVCCM Taifa alisema,"Ni kweli tumemkamata tangu jana usiku tumekesha tukifanya uchunguzi wa kina kuhusu swala hill, nitatoa taarifa baadaye kuhusu tukio hilo".

No comments:
Post a Comment