Waziri kivuli wa mambo ya ndani ya nchi Mhe Godbless Lema amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa.
Pia Mhe Lema amemshauri Rais Magufuli kuwaangalia mahabusu waliokaa muda mrefu gerezani pasipo kupata haki zao.
Katika maadhimisho ya Uhuru kwa Tanganyika (Tanzania bara) jana jumamosi Desemba 9,2071 mkoani Dodoma Rais Magufuli alitoa msamaha wa wafungwa 8,157 kati ya hao 1,828 waliachia uhuru kuanzia jana.
Pia leo jumapili Desemba 10, 2017 Rais Magufuli ametia saini nyaraka za msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha ambao ni Nguza Viking (babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha).
Akizungumza na kulunzifikra blog Mhe Lema amesema mateso wanayoyapata mahabusu yanahitaji kuangaliwa na Rais Magufuli.
"Rais Magufuli, Mungu akubariki sana kwa msamaha uliotoa jana kwa wafungwa na hasa waliokaa magerezani kwa muda mrefu pamoja na wazee, msamaha ni baada", amesema Mhe Lema.
"Ni msamaha muhimu meal, mtu aliyehukumiwa maisha au kifo alipata msamaha ni jambo jema sana,nimefurahi sana, wamesamehewa sasa hawatakuwa tena magerezani maisha yao yote", amesema Mhe Lema.
" Nimefurahia sana kwamba hata wale waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa hasa wazee pia wamepata msamaha huo kwangu naona ni jambo jema sana na zuri kwa MTU anayejua huzuni ya magerezani atakubaliana nani",alisema Mhe Lema.
Kuhusu mahabusu Mhe Lema amesema "wako mahabusu wamekuwa magerezani kwa muda mrefu bila kesi zao kukamilika kwa wakati. Namuomba Rais Magufuli kufuatilia na watu kama hasa pia".

No comments:
Post a Comment