Mwili wa mwandishi wa habari mwandamizi, Joyce Mmasi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita unatarajiwa kuagwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana na kamati ya mazishi ya mwandishi huyo wa zamani wa magazeti ya Mwananchi imeeleza kuwa shughuli za kuaga zitaanza saa nne asubuhi na kukamilika saa saba mchana na baada ya hapo mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Mbokomu, Moshi kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
Shughuli hiyo ya kuuaga mwili wa marehemu Joyce aliyefariki dunia katika Hospitali ya TMJ baada ya kuugua kwa muda mfupi inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wanahabari na wananchi ambao walishirikiana naye katika uhai wake.
Kifo chake
Joyce alifariki dunia saa 10 alfajiri Jumatano iliyopita na kwa mujibu wa mumewe, Andrew Kamugisha, kifo chake kilitokana na maradhi ya saratani ya damu na kwamba kutokana na tatizo hilo, mwili ulishindwa kutengeneza damu ikiwamo rojorojo katika mifupa (bone marrow) na hivyo kusababisha mfumo wa chembe hai kutofanya kazi inavyotakiwa hali iliyosababisha aongezewe damu mara kadhaa.
Joyce alizaliwa Juni 18, 1978 mkoani Kilimanjaro. Alisoma Shule ya Msingi Mbokomu na kisha Sekondari ya Kimbo kabla ya kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro kwa masomo ya diploma.
Baada ya kuhitimu masomo hayo mwaka 1995, alijiunga na Kampuni ya Business Times akiandikia gazeti la Majira hadi mwaka 2000 alipohamia Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), kabla ya kwenda nchini Uganda kwa masomo ya Shahada ya Kwanza ya Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Kampala (Kiu).
Aliporejea nchini aliendelea kufanya kazi MCL akiwa mwandishi mwandamizi wa habari za siasa kabla ya kuacha kwa hiari yake Machi, 2017 na kujikita katika ujasiriamali na masomo ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Dar es Salaam hadi alipofariki dunia.

No comments:
Post a Comment